Timu ya taifa ya soka ya Kenya kwa wanawake ,Harambee Stars imeanza mazoezi ya wiki huko Miramas Ufaransa, kujiandaa kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON) kuanzia Julai 26 nchini Morocco.
Starlets watafungua kipute cha WAFCON Julai 26 dhidi ya wenyeji Morocco, kundini A,kabla ya kukabiliana na Algeria na Senegal.
Kenya inayofunzwa na Beldine Odemba, itakuwa ikishirki Kombe la Dunia mwaka huu kwa mara ya pili tangu ilipocheza kwa mara ya kwanza mwaka 2016.
Timu sita bora kwenye mashindano ya mwaka huu zikiwemo nne za nusu fainali zitafuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao nchini Brazil.