Serikali kuchunguza visa vya uhuni Ol Kalou

Waziri ameahidi Usalama wa kutosha wakati wa uchaguzi huo mdogo huku maafisa wa polisi wa kutosha wakitumwa kushika doria.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, amesema serikali itachunguza visa vya machafuko vilivyoshuhudiwa katika uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Olkalou siku ya Alhamisi.

Murkomen amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu kisa ambacho watu wanaodaiwa kuvalia nguo zisizo rasmi na kuwashambulia raia kwa vitoza machozi.

Waziri ameahidi usalama wa kutosha wakati wa uchaguzi huo mdogo huku maafisa wa polisi wa kutosha wakitumwa kushika doria.

Murkomen alikuwa akizungumza siku ya Alhamisi baada ya kuhutubia bunge la kaunti ya Trans Nzoia .

Share This Article