Makala ya 23 ya kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia yanarejea leo Jumatano Julai 14, kwa nusu fainali ya kwanza kati ya mabingwa mara mbili Ufaransa na mabingwa wa mwaka 2010 Uhispania.
Nusu fainali hiyo itachezwa uwanjani Dallas,Marekani kuanzia saa nne usiku,huku kipute hicho kikirejea baada ya mapumziko ya siku mbili.
Ufaransa wanaoorodheshwa wa kwanza Duniani wamecheza fainali 4 kati ya saba za hivi punde katika historia ya Kombe la Dunia,wakitwaa ubingwa mwaka 1998 na 2018, huku wakipoteza fainalini 2006 na 2022.
Pambano la leo litakuwa la 39 baina ya miamba hao wawili,Uhispania wakishinda 18,Ufaransa wakashinda 13 na saba kumalizikia sare.
Ufaransa iliwashinda Uhispania 2-1 katika fainali ya UEFA Nations League mwaka 2021,kabla ya Uhispania kulipiza kisasi na kuwabwaga Ufaransa kwenye nusu fainali ya Kombe la Euro mwaka 2024, na kuilaza tena Ufaransa nusu fainalini ya Kombe la UEFA Nations League mwaka 2025.
Ufaransa itatagemea pakubwa ushirikiano wa Ousman Dembele na Kylian Mbappe, anayeongoza ufungaji mabao kwa magoli manane, wakati Uhispania ikitegemea huduma za Rodri na chipukizi Lamine Yamal.
Mshindi atacheza fainali ya Jumapili hii ,huku atakayeshindwa akisubiri kucheza mechi ya nafasi ya tatu na nne, Jumamosi usiku dhidi ya mshinde wa semi fainali ya pili baina ya mabingwa watetezi Argentina dhidi ya Uingereza kesho.
Mechi 100 zimepigwa kufikia sasa kwenye kipute cha Kombe la Dunia na mabao 292 kufungwa.