Rais wa Uganda Yoweri Museveni anapanga kukutana na wafalme na machifu kujadili mustakabali wa taifa hilo la Afrika Mashariki.
Haya yalifichuliwa na Makamu wa Rais Jessica Alupo aliyesema kwamba Rais Museveni anataka kukutana na viongozi wote wakitamaduni kuzungumza kuhusu jinsi ya kushirikiana kama viongozi, kuboresha maisha ya raia.
Alupo alitoa taarifa hizi katika kikao maalum na baraza la mawaziri la ufalme wa Buganda Julai 7, 2026.
Makamu huyo wa Rais alimfahamisha kiongozi mkuu wa ufalme wa Buganda Charles Peter Mayiga kwamba Rais anapanga kuanzisha mazungumza na machifu ili kuanzisha mdahalo.
“Baada ya kukutana na machifu wa Buganda, Rais atatenga siku nyingine maalumu ya kukutana na viongozi wote wa kitamaduni nchini Uganda kujadili mustakabali wa nchi yetu na namna ya kushirikiana kama viongozi kwa manufaa ya wananchi wote wa Uganda,” Alisema Alupo.
Kiongozi wa Buganda Owek. Mayiga alikaribisha mazungumzo hayo akisema Ufalme wa Buganda ni makazi ya watu wote wa Uganda, hivyo ni muhimu huduma ziwafikie wananchi wote.
“Tuko tayari kushirikiana na serikali kuu katika programu mbalimbali zinazowagusa moja kwa moja wananchi wa Buganda. Ufalme wa Buganda una watu wa makabila na maeneo mbalimbali; karibu kila Muganda na Mugaanda mwingine kutoka sehemu yoyote ya Uganda anaishi hapa. Hivyo, huduma zinapowafikia wananchi wa Buganda, Waganda na Waganda wengine wote wa Uganda hunufaika pia,” alisema.