Mwanamuziki wa Tanzania, Zuchu, amekanusha uvumi ulioenezwa mitandaoni kwamba amekuwa mjamzito na amejifungua kisiri.
Mke huyo wa mwanamuziki mwenza Diamond Platnumz alidaiwa kuwa mjamzito hasa baada yake kuonekana hadharani akiwa ameongeza uzani wa mwili na akiwa anavaa mavazi makumbwa makubwa.
Uvumi huo ulizua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wake, huku baadhi ya watu wakidai kuwa Msanii huyo alikuwa ameficha ujauzito wake na hata kujifungua bila kuweka taarifa hadharani.
Akizungumza kupitia akaunti zake za mitandao kijamii, Zuchu alikanusha taarifa hizo kwa njia ya utani, akionyesha kushangazwa na habari hizo ambazo alisema hana taarifa nazo.
“Nilisikia kwamba nimejifungua, wakati mimi mwenyewe sina taarifa yoyote kuhusu jambo hilo. Ngoja kwanza nitoe taarifa nikiwa bado kazini, nawaomba msikilize wimbo wa Chinga wa Ibraah,” aliandika Zuchu.
Kauli hiyo imezua hisia tofauti kwa mashabiki wake, huku wengi wakichukulia ujumbe huo kama njia ya kuweka wazi kuwa taarifa zilizokuwa zikisambazwa hazikuwa na ukweli wowote.
Hadi sasa, Zuchu hajathibitisha uwepo wa ujauzito wala kujifungua, na hivyo uvumi huo unaendelea kubaki kuwa mada inayozungumzwa zaidi mitandaoni bila ushahidi rasmi.