Simba wa Atlas,Morocco, wafuzu robo fainali Kombe la Dunia

Aidha, Morocco ni timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia mara mbili mtawalia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Atlas Lions ya Morocco, ndio timu ya kwanza kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka huu, baada ya kuwalabua wenyeji wenza Canada magoli 3-0, katika mechi ya kwanza ya raundi ya 16 Jumamosi usiku mjini Houston.

Azzedine Ounahi alipachika mabao mawili naye Soufiane Rahimi, akaongeza moja  yote katika kipindi cha pili,na kuwahakikishia Simba wa Atlas nafasi katika robo fainali kwa mara ya pili mtawalia.

Aidha, Morocco ni timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia mara mbili mtawalia.

Share This Article