Mbappe apiga mawili na kuibeba Ufaransa hadi hatua ya 16

Mbappe alifikisha idadi ya magoli 18 aliyofunga katika Kombe la Dunia, moja nyuma ya Lionel Messi, na pia kumfikia Messi katika ufungaji bora mwaka huu kwa mabao 6.

Dismas Otuke
1 Min Read

Nahodha Kylian Mbappe aliendelea kudhihirisha ubora wake alipopachika magoli mawili na kuisaidia Ufaransa kuwanyuka Uswidi magoli 3-0 katika mechi ya sita ya raundi ya 32 usiku wa kuamkia leo ugani New York jijini New Jersey nchini Marekani.

Mbappe alipiga goli la kwanza dakika ya 43, akiunganisha krosi ya Ousman Dembele wakati The Blues wakiongoza kuelekea mapumzikoni licha ya Waswidi kujihami kwa kila hali kuzima mashambulizi.

Bradely Barcola alitanua uongozi wa vijana wa Didier Deschamps baada ya kushirikiana vyema na Michael Olise kabla ya kutoa pasi nyingine kwa Mbappe aliyepifa goli la tatu kunako dakika ya 74.

Mbappe alifikisha idadi ya magoli 18 aliyofunga katika Kombe la Dunia, moja nyuma ya Lionel Messi, na pia kumfikia Messi katika ufungaji bora mwaka huu kwa mabao 6.

Ufaransa wataelekea uwanjani Philadelphia, Marekani Jumamosi hii dhidi ya Paraguay katika mechi ya raundi ya 16, wakiendeleza sakasaka zao za kombe la tatu la Dunia.

Share This Article