Miradi mbalimbali ya maendeleo inaendelea kutekelezwa na serikali ya Kenya Kwanza kila pembe ya nchi, miaka minne tangu serikali hiyo ilipoingia madarakani.
Katibu katika Wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo amesema maendeleo yanayotekelezwa na utawala wa sasa yanadhihirika kwa wote.
“Hakuna sehemu ya nchi hii unayoweza kutembelea leo hii bila kuona maendeleo bayana kupitia mipango na miradi ya serikali,” amesema Dkt. Omollo.
“Najivunia mafanikio ambayo tumefikia kwa niaba ya nchi hii chini ya uongozi wa Rais William Ruto.”
Matamshi ya Dkt. Omollo yanakuja wakati ambapo Rais Ruto ameahidi kuwa serikali itatekeleza ahadi zote ilizowaahidi Wakenya wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Ruto aliyasema hayo jana Jumatatu wakati wa uzinduzi wa barabara ya juu ya Ngong-Naivasha iliyopo katika eneo bunge la Dagoretti Kusini.
Ruto alielezea imani kwamba uzinduzi wa barabara hiyo utasaidia mno kupunguza msongamano wa magari jijini Nairobi.
Upinzani umekuwa mstari wa mbele kwa kuikosoa serikali ya Kenya Kwanza kwa kushindwa kutekeleza miradi mbalimbali iliyoawaahidi Wakenya wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.