Simba wa Atlas kupimana ubabe na Orange ya Uholanzi, mapema Jumanne

Timu zote mbili zilimaliza mechi za makundi kwa alama sawa saba ,kushinda michuano miwili na kutoka sare mmoja,Uholanzi wakiongoza kundi F nao Morocco, wakachukua nafasi ya pili kundini C.

Dismas Otuke
1 Min Read

Miamba wa Afrika Morocco almaarufu Atlas Lions watakuwa na kibarua kigumu watakaposhuka uwanjani Monterrey nchini Mexico, Jumanne saa kumi alfajiri dhidi ya Orange ya Uholanzi, kwa mechi ya nne ya raundi ya 32 ya Kombe la Dunia.

Itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana katika Kombe la Dunia baada ya Uholanzi kuishinda Morocco mabao 2-1 mwaka 1994.

Timu zote mbili zilimaliza mechi za makundi kwa alama sawa saba ,kushinda michuano miwili na kutoka sare mmoja,Uholanzi wakiongoza kundi F nao Morocco, wakachukua nafasi ya pili kundini C.

Uholanzi ilitoka sare ya 2-2 na Japan kabla ya kuwashinda Uswidi 5-1,na hatimaye kuikomoa  Tunisia 3-1.

Morocco pia walifungua  kwa sare ya bao moja dhidi Brazil kabla ya kuipiku Scotland goli moja kwa nunge na kisha kuizaba Curacao  4-2.

Mshindi wa mechi hiyo atakumbana na Canada Jumapili hii mjini Houston,Marekani katika raundi ya 16 bora.

Share This Article