Limbukeni Cape Verde,Senegal,Misri na Ghana zimefuzu kwa awamu ya 32 bora ya Kombe la Dunia, siku moja kabla ya kukamilika kwa mechi za makundi.
Cape Verde ilifuzu kufuatia sare tasa dhidi ya Saudi Arabia, katika kundi H na kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Uhispania, iliyoongoza kwa alama saba baada ya kuwalaza Uruguay, bao moja kwa bila katika mechi nyingine ya mwisho mapema Jumamosi.
Mabingwa mara saba wa Afrika,Misri ,walimaliza katika nafasi ya pili kundini G, kufuatia sare ya bao moja dhidi ya Iran, katika mechi ya mwisho wakizoa alama 5 sawa na viongozi wa kundi hilo Ubelgiji ,waliowalabua New Zealand 5-1.
Senegal wamefuzu kama mojawapowa timu bora katika nafasi ya tatu hususan baada ya Cape Verde, kutoka sare tasa na Saudi Arabia.
Ghana ambao watacheza mechi ya mwisho ya kundi L dhidi ya Croatia, mapema Jumapili wamefuzu bila kugusa mpira kwani alama 4 walizo nazo zinawafuzisha moja kwa moja.