Wawakilishi wa Afrika, Ivory Coast walihitaji mabao mawili ya Nicholas Pepe moja katika kila kipindi ili kufuzu kwa awamu ya 32 waposajili ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya limbukeni Curao, Alhamisi usiku.
Ushindi huo uliwaweka tembo wa Ivory Coast katika nafasi ya pili kwa pointi sita sawia na viongozi Ujerumani, licha ya kuambulia kichapo cha 2-1 kutoka Ecuador katika mechi nyingine ya mwisho kundini E.
Kundini F mapema Ijumaa, Uswidi imetoka sare ya bao moja na Japani na kufuzu kwa raundi ya 32 bora, nao Uholanzi wakaongoza kundi hilo baada ya kuwalemea Tunisia mabao 3-1.
Katika kundi D, Marekani ambayo tayari ilikuwa imejihakikishia nafasi ya kwanza ilipigwa magoli 3-2 nyumbani na Uturuki ambao tayari wameyaaga mashindano huku Paraguay na Australia zikitoka sare tasa, matokeo yaliyozivusha timu zote kwa raundi ya 32 bora.