Afrika Kusini imefuzu kwa raundi ya 32 bora kwa mara ya kwanza baada ya kuwashinda Korea Kusini bao moja kwa bila mapema Alhamisi na kumaliza wa pili kundini A kwa alama 4.
Bafana Bafana walihitaji bao la Thapelo Maseko la kipindi cha pili katika dakika ya 63 ili kuandiskisha historia hiyo.
Afrika Kusini sasa watamenyana na waandalizi wenza Canada katika raundi ya 32 bora Jumapili usiku mjini Los Angeles nchini Marekani.