Morocco ndiyo timu ya kwanza ya Afrika kufuzu kwa awamu ya 32 bora ya kipute cha Kombe la Dunia ambacho kimeingia wiki ya pili nchini Marekani, Canada na Mexico.
Morocco ilimaliza ya pili kundini C kwa pointi 7 kwa kutoka sare na Brazil na kuzishinda Scotland na Haiti.
Atlas Lions waliocheza hadi nusu fainali ya mwaka 2022 nchini Qatar, watakumbana na aidha Uholanzi, Japani au Uswidi katika mechi ya awamu ya 32 bora.
Timu nyingine za Afrika zilizo katika nafasi ya kusonga mbele ni Misri, Ivory Coast, Ghana, Algeria, Cape Verde na DRC.
Mechi za makundi zitakamilika Jumapili hii.
Makundi ya D, E na F yatakamilisha mechi zao leo Alhamisi ili kubaini timu ziatakazofuzu kwa raundi ya 32 bora.