Vijana washauriwa kujiepusha na wanasiasa wanaowapotosha

Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula amewahimiza vijana kuzingatia elimu kama uwekezaji wa kibinafsi, ulio na manufaa mengi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Moses Wetang'ula - Spika wa Bunge la Taifa.

Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula, amewahimiza vijana kuzingatia mustakabli wao kupitia elimu, biashara na kilimo, akiwaonya dhidi ya kutumiwa na wanasiasa wenye masilahi ya kibinafsi.

Akizungumza kwenye mkutano na wazee pamoja na wasomi katika eneo bunge la Tongaren ulioongozwa na mbunge wa eneo hilo John Chikati, Wetang’ula alitoa wito kwa vijana kuzingatia elimu kama uwekezaji wa kibinafsi, ulio na manufaa mengi.

“Nawahimiza vijana kuwa viongozi wa maisha yao, baada ya elimu, anayefaidika ni wewe. Hampo shuleni kwa sababu ya mtu yeyote, lakini kwa ajili yako,” alisema Wetang’ula.

Spika huyo alidokeza kuwa vijana wengi huwa hawadhamini mageuzi ya elimu na taaluma wanayopata, ikizingatiwa kuwa maamuzi wanayotekeleza leo yataathiri fursa zao za siku zijazo.

Aliwahimiza wanafunzi kuzingatia kwa makini elimu na kukumbatia uvumbuzi.

Share This Article