Desert Foxes ya Algeria ilisajili ushindi wa kwanza katika historia yao ya Kombe la Dunia baada ya kutoka nyuma na kuwashinda limbukeni Jordan mabao 2-1 mapema Jumanne katika kundi I.
Al Rashdan alifunga bao la kwanza kwa Jordan katika dakika ya 36 huku wakiongoza kuelekea mapumzikoni.
Nadhir Benbouali aliwanusuru Algeria kwa bao la kusawazisha katika dakika ya 69, naye Amine Gouiri akafunga la pili dakika ya 82, ushindi unaofufua matumaini yao ya kufuzu kwa awamu ya 32 bora.
Hata hivyo, Jordan wameyaaga mashindano baada ya kushindwa mechi mbili.