Uhispania imesajili ushindi wa kwanza katika Kombe la Dunia mwaka huu baada kuwachabanga Saudi Arabia mabao 4-0, katika mechi ya kundi H, ugani Mercedes Benz Jumapili jioni.
Lamine Yamal alitikisa wavu kwa goli la kwanza dakika ya 10 ,kabla ya Mikel Oyarzabal, kuongeza la pili dakika ya 21 na la tatu dakika tatu baadaye.
Hassan Tambakti alijifunga kunako kipindi cha pili.
Uhispania wanaongoza kundi hilo kwa alama 4.