IGAD yatoa wito wa kuheshimiwa kwa Somalia

IGAD imesema inafuatilia ripoti kuhusu kufunguliwa kwa ubalozi wa Somaliland Jijini Jerusalem, Israel.

Tom Mathinji
1 Min Read
IGAD yatoa wito wa kuheshimiwa kwa Jamhuri ya Somalia.

Shirika la Maendeleo ya Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki (IGAD), limeelezea kujitolea kudumisha ahadi yake ya kulinda mamlaka, umoja, maadili ya mipaka na uhuru wa kisiasa wa Jamhuri ya Somalia kuambatana na mkataba wa IGAD, katiba ya Umoja wa Afrika na makubaliano ya Umoja wa Mataifa.

Kwenye taarifa, shirika hilo la IGAD limesema linafuatilia ripoti kuhusu kufunguliwa kwa ubalozi wa Somaliland Jijini Jerusalem, Israel, huku ikirejelea msimamo wake wa muda mrefu kwamba, umoja wa Somalia na maadili ya mipaka lazima uheshimiwe.

Aidha, IGAD imeelezea wasiwasi dhidi ya hatua zozote zinazohujumu uhuru, umoja na mipaka ya jamhuri ya Somalia, likionya kuwa hatua kama hizo huenda zikasababisha taharuki, amani ya kikanda, udhabiti na ushirikiano.

Taarifa hiyo ya IGAD inajiri baada ya ziara ya Rais wa Somaliland Abdirahman Mohamed Abdullahi nchini Israel, ambako alifungua ubalozi wa Somaliland Jijini Jerusalem na kushiriki mazungumzo na Maafisa Wakuu wa Israeel, akiwemo Waziri Mkuu Benjamin na wanachama wa Knesset.

Kwenye mkutano huo, viongozi hao wawili waliangazia ukuaji wa uhusiano kati ya Israel na eneo hilo la Somaliland ambalo limejitenga kutoka kwa Somalia.

Share This Article