Canada wainyeshea Qatar, wanusia raundi ya pili

Jonathan David alipachika hat trick na kujiunga na Lionel Messi katika orodha wafungaji bora.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waaandalizi wenza wa kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia Canada, walijiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa kwa awamu ya 32 bora baada ya kuinyofoa Qatar kwa mabao 6-0 katika mchuano wa kundi B mjini Vancouver, Canada Alhamisi usiku.

Jonathan David alipachika hat trick na kujiunga na Lionel Messi katika orodha ya wafungaji bora.

Cyle Larin na Nathan Saliba waliongeza goli moja kila mmoja huku Mohammad Al Mannai akijifunga.

Canada watahitimisha ratiba dhidi ya Uswizi Jumanne ijayo katika mechi ya mwisho itakayoamua viongozi wa kundi hilo.

Uswizi waliweka hai matumaini ya kufuzu kwa raundi ya 32 bora, baada ya kuibinikiza Bosnia Herzegovina magoli 4-1 katika mechi ya Alhamisi usiku.

Share This Article