Afrika Kusini maarufu kama Bafana Babafana, wanakabiliwa na hatari ya kuaga fainali za Kombe la Dunia mwaka huu katika hatua ya makundi, baada ya kwenda sare ya bao moja na Czechia katika mechi ya pili ya kundi A Alhamisi jioni.
Michal Sadilek aliwaweka Czechia kifua mbele kunako dakika ya sita katika pambano hilo uwanjani Mercede Benz mjini Atlanta nchini Marekani.
Teboho Mokoena aliwaepushia Afrika Kusini fedheha kwa goli la kusawazisha dakika ya 83 kupitia mkwaju wa penalti.
Afrika Kusini ni sharti washinde mechi ya mwisho dhidi ya Korea Kusini Jumanne ijayo ili kufuzu kwa raundi ya 32 bora.
Czechia, watahitimisha mechi za makundi pia Jumanne dhidi ya wenyeji Mexico, ambao tayari wamefuzu kwa awamu ya 32 bora.