Bunge la Taifa lapitisha Mswada wa Fedha 2026

Wabunge 122 walipiga kura kuunga mkono mswada huo, huku wabunge 40 wakiupinga.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kikao cha Bunge la Taifa.

Bunge la Taifa limepitisha Mswada wa Fedha wa mwaka 2026, huku  sasa ukisubiri kuwasilishwa kwa Rais ili atie saini kuwa sheria.

Wabunge 122 walipiga kura kuunga mkono mswada huo, huku wabunge 40 wakiupinga.

Hata hivyo, mswada huo ulipitishwa baada ya vipengee kadhaa kufanyiwa marekebisho yaliyopendekezwa na kamati ya Bunge la Taifa kuhusu Fedha na Mipango ya Taifa.

Marekebisho hayo yalijumuisha kuondolewa au kufanyiwa marekebisho kwa mapendekezo kadhaa ya ushuru ambayo yalipingwa na wafanyabiashara, makundi ya kijamii na wananchi.

Serikali ilimeshikilia kuwa mswada huo unalenga kuimarisha ukusanyaji wa mapato, huku ikiepuka ushuru utakaosababisha kuongezeka kwa gharama ya maisha.

Kupitishwa kwa mswada huo kunajiri baada ya wiki kadha za mijadala bungeni, huku wabunge wakipigia kurunzi mikakati ya ushuru na mapato iliyopendekezwa na serikali.

Share This Article