Nahodha wa mabingwa watetezi Argentina Lionel Messi anaongoza chati ya ufungaji mabao katika fainali za Kombe la Dunia kufuatia kukamilika kwa mechi 24 za mzunguko wa kwanza hatua ya makundi.
Messi amepachika mabao 3 ambayo pia ilikuwa hat trick ya kwanza kwenye fainali za mwaka huu walipokuwa wakicheza na Algeria.
Wanandinga wengine saba wamefunga magoli 2 kila mmoja wakiwemo; Kylian Mbappe wa Ufaransa, Erling Halaand wa Norway, Elijah Henry Just wa Newzealand, Yasin Ayari wa Uswidi, Kai Havertz wa Ujerumani, Folarin Balogun wa Marekani na Hary Kane wa Uingereza.

Jumla ya mabao 75 yamefungwa ikiwa wastani wa magoli 3 kwa kila mechi.
Wachezaji watatu wamelishwa kadi nyekundu wakiwemo wawili wa Afrika Kusini (Sphephelo Sithole na Themba Zwane) na mmoja wa Mexico (César Montes) huku mabao ya kujifunga yakiwa matano.
Mashabiki waliofika uwanjani kushuhudia mechi baada ya mzunguko wa kwanza ni 1,572,584, ikiwa wastani wa mashabiki 65,524 kwa kila mchuano.