Chui wa Congo wakataa kulala chali dhidi ya Ureno

DRC walikuwa wakirejea kwenye fainali za Kombe la Dunia baada ya kuwa nje kwa miaka 52.

Dismas Otuke
1 Min Read

Chui wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametoka nyuma bao moja na kunusuru pointi moja dhidi ya Ureno, katika mchuano wa ufunguzi wa kundi K, uliopigwa uwanjani Houston,Marekani Jumatano jioni.

Ureno walichukua uongizi wa mechi hiyo mapema kupitia kwa goli la João Neves, huku Yoane Wisa, akikomboa kwa DRC mwishoni mwa kipindi cha kwanza kupitia kwa kichwa.

DRC walikuwa wakirejea kwenye fainali za Kombe la Dunia baada ya kuwa nje kwa miaka 52.

Nahodha wa Ureno,Cristiano Romnaldo aliyekuwa akishiriki fainali za Komb la Dunia kwa mara ya sita alimaliza dakika zote 90.

Share This Article