Shirikisho la soka nchini Tunisia linamtafuta kocha mpya baada ya kumtimua Sabri Lamouchi Jumatatu, kufuatia kipoigo cha mabao 5-1, katika mechi ya ufunguzi ya kundi F mjini Monterrey,Mexico.
Mondher Kebaier,aliteuliwa kaimu kocha wa kutwaa nafasi ya Lamouchi aliye na umri wa miaka 54, mzawa wa Ufaransa.
Yamkini Shirikisho la soka nchini Tunisia linatafakari kumteua Herve Renard.

Tunisia watacheza na Japana katika mechi ya pili kabla ya kukamilisha ratiba dhidi ya Uholanzi.