Wenyeji wenza wa fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia walifungua kampeini yao kwa kishindo baada ya kuilabua Paraguay mwabao 4-1,katka mechi ya kundi D, iliyopigwa mapema Jumamosi katika uwanja wa Los Angeles.
Folarin Balogun, alipachika mabao mawili kunako kipindi cha kwanza huku Damian Bobadilla, akijifunga katika mchuano ambao Marekani waliongoza mabao 3-0 kufikia mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Marekani ukipenda the Stars and Stripes waliendelea kutawala mechi katika kipindi cha pili huku Giovanni Reyna, akiongeza la nne naye Mauricio, akapachika goli la kufutia machozi kwa wageni Paraguay.

Sawia na Mexico na Canada ,Marekani pia ilifanya sherehe za ufunguzi huku burudani ikiporomoshwa na wasanii Katy Perry, LISA, Anitta, Tyla, Rema, Future, Dan + Shay na Purahei Soul.