FIFA World Cup:Korea yatoka nyuma na kuizima Czechia

Mexico wanaongoza kundi  A kwa pointi 3 sawia na Czechia walio katika nafasi ya pili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Korea Kusini imetoka nyuma bao moja kwa bila na kusajili ushindi wa mabao 2-1, katika mchuano wa pili wa Kombe la Dunia uliopigwa mapema Ijumaa katika uchanjaa wa Guadarajala.

Kipindi cha kwanza kilimazikia sare tasa kabla ya Ladislav KREJCI kuwaweka Czechia uongozini kunako dakika ya 59.

HWANG Inbeom alikomboa kwa Korea Kusini dakika ya 69 huku OH Hyeongyu, akipiga la ushindi dakika 10, kabla ya kipenga cha mwisho.

Mexico wanaongoza kundi  A kwa pointi 3 sawia na Czechia walio katika nafasi ya pili.

Share This Article