Watu 12 wafariki kwenye shambulizi la risasi Afrika kusini

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 12 wafariki kwenye shambulizi la risasi Afrika Kusini.

Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki, walivamia eneo la Cleveland  karibu na mji  wa Johannesburg na kuwapiga risasi watu ambapo 12 walifariki na wengine 9 kujeruhiwa.

Kulingana na msemaji wa polisi wa Afrika Kusini Kanali Dimakatso Nevhuhulwi, zaidi ya watu 10 walitekeleza shambulizi hilo saa tano usiku saa za nchini hiyo.

“Wanaume wanane na wanawake watatu, walitangazwa wamefariki katika eneo la mkasa,” alisema Nevhuhulwi,

Kulingana na msemaji huyo wa polisi, wavamizi hao katika eneo hilo na kuwafyetulia wakazi risasi kabla ya kutoroka eneo hilo wakitumia magari.

Idara ya Polisi imesema imeanzisha uchunguzi kuhusiana na shambulizi hilo ikiwalenga washukiwa 10, huku chanzo cha shambulizi hilo kikisalia kitendawili.

Share This Article