Difenda wa zamani wa timu ya taifa Harambee Starlets Terry Ouko, ameteuliwa kusimamia mechi zitakazochezwa katika uwanja wa Mercedes-Benz mjini Atlanta nchini Marekani.
Ouko atasimamia na kuhakikisha viwango vya FIFA kuhusu haki za kibinadamu, kukabiliana na ubaguzi na utunzaji mazingira katika mechi tano za makundi na tatu za mwondoano zitakazochezwa katika uwanja huo.
Ouko kwa sasa anahudumu kama Naibu Rais wa chama cha maslahi ya wachezaji (KEFWA), kando na kuketi katika bodi ya kimataifa ya FIFA (FIFPRO).
Mechi za makundi zitakazochezwa uwanjani Mercede Benz nchini Marekani
Juni 15: Spain vs Cape Verde
Juni 18: South Africa vs Czechia
Juni 21: Spain vs Saudi Arabia
Juni 24: Morocco vs Haiti
Juni 27: Uzbekistan vs DR Congo
Uga huo aidha utaandaa mechi moja ya raundi ya 32, moja ya raundi ya 16 na nusu fainali moja.