Malimbukeni wanaoshiriki Kombe la Dunia mwaka huu

Aidha, kwa mara ya kwanza, timu 48 zinashiriki ikiwa ongezeko kutoka idadi ya awali ya mataifa 32.

Dismas Otuke
1 Min Read
Mashabiki wa Cape Verde wakiikaribisha timu yao mjini Boston,Marekani

Fainali za 23 za Kombe la Dunia zimeratibiwa kuanza rasmi kesho kutwa Juni 11 kwa mechi ya ufunguzi ya kundi A kati ya Mexico na Afrika Kusini.

Kipute hicho kinaandaliwa na mataifa matatu kwa mara ya kwanza; Mexico, Marekani na Canada.

Aidha, kwa mara ya kwanza, timu 48 zinashiriki ikiwa ongezeko kutoka idadi ya awali ya mataifa 32.

Mataifa manne ya Cape Verde ya Afrika, Curacao kutoka CONCACAF na wawakilishi wawili kutoka Asia, Jordan na Uzbekistan yatakuwa yakishiriki kwa mara ya kwanza kwenye fainali za mwaka huu.

Curacao imejumuishwa kundi E katika fainali za mwaka huu pamoja na mabingwa mara nne Ujerumani, Ivory Coast na Ecuador.

Cape Verde maarufu Blue Sharks, watacheza kundini H na mabingwa wa mwaka 2010, Uhispania, Uruguay na Saudi Arabia.

Jordan watakuwa na kibarua kundini J pamoja na mabingwa watetezi Argentina, Algeria na Austria.

Uzbekistan nao wataanza safari yao ya Kombe la Dunia pamoja na Ureno, Colombia na DR Congo wanaorejea baada ya kuwa nje kwa miaka 52.

 

 

 

Share This Article