DRC yamteua Gavana mpya wa Ituri

Tom Mathinji
1 Min Read
DRC yamchagua Gavana Mpya wa Ituri.

Wilaya ya Ituri ambayo ndiyo kitovu cha mlipuko wa ugonjwa wa Ebola,  sasa ina Gavana mpya huku juhudi zikiimarishwa kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

Rais wa taifa hilo Felix Tshisekedi, amemteua Meja Jenerali Kasongo Mulumba Batoka Gaby kuwa Gavana mpya waIturi na kuchukua mahala pa Luteni Jenerali Johnny Luboya Nkashama.

shesekedi ametanganza mabadiliko hayo leo Jumamosi, kupitia runinga ya taifa, huku gavana huyo mpya akitarajiwa kifanikisha juhudi za kudhibiti msambao wa ugonjwa huo.

Hadi kufikia sasa visa zaidi ya 400 vimethibitishwa nchini DRC, huku Ituri ikiwa na idadi kubwa zaidi. Watu zaidi ya 80 wamefariki kutokana na makali ya ugonjwa.

Hata hivyo, watu wanne wamepona ugonjwa huo nchini DRC, hii ikiwa ni afueni kubwa katika vita dhidi ya ugonjwa huo.

WHO imesema bado dawa ya kutibu ugonjwa huo haijapatikana, huku ikitoa wito wa juhudiz za pamoja katika kukabiliana na msambao wake.

Share This Article