Waiguru awasihi wakazi wa Ol Kalou kumchagua mwaniaji wa UDA

Tom Mathinji
1 Min Read

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, ametoa wito kwa wakazi wa Ol Kalou kumchagua mwaniaji wa chama cha UDA Sammy Muchina Nyaga katika Uchaguzi mdogo ujao.

Akizungumza alipokuwa akimpigia debe Muchina,  Gavana Waiguru alisema mwaniaji huyo alishirikiana kwa karibu na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo marehemu David Kiaraho kwa miradi ya maendeleo katika eneo bunge hilo.

Alidokeza kuwa eneo bunge la Ol Kalou litanufaika pakubwa iwapo litamchagua kiongozi ambaye atashirikiana kwa karibu na serikali.

Kiongozi huyo wa Kirinyaga aliwashauri wapiga kura kuweka mbele miradi ya maendeleo na kuepuka ahadi za uwongo kutoka kwa baadhi ya wanasiasa.

Kwenye mkutano huo, Waiguru alikuwa ameandamana na aliyekuwa waziri Moses Kuria, wabunge  Jane Kagiri (Laikipia), Michael Muchira (Ol Jororok), James Githua (Kabete) na Kwenya Thuku (Kinangop).

Share This Article