Maafisa wa Umma kushtakiwa kwa uhalifu baada ya jengo kuporomoka South C

Tom Mathinji
1 Min Read

Kiongozi wa Mashtaka ya Umma, ameidhinisha mashtaka ya uhalifu dhidi ya maafisa wa umma, wastawishaji na wataalam kadhaa kuhusiana na jengo la Manzil lililoporomoka katika mtaa wa South C Januari 2, 2026.

Kwenye taarifa kwa wanahabari, afisi ya kiongozi wa Mashtaka ya Umma imethibitisha kupokea ripoti ya uchunguzi kutoka kwa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), na kubaini Kuna ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashtaka maafisa hao.

Miongoni mwa wale watakaofunguliwa mashtaka ni pamoja na Patrick Analo Akivaga, anayekabiliwa na mashtaka mawili ya utumizi mbaya wa mamlaka na utepetevu wa majukumu.

Afisi hiyo ya kiongozi wa Mashtaka ya Umma pia iliwafungulia mashtaka maafisa kadhaa wa umma, wastawishaji na taasisi za wataalam kuhusiana na kuporomoka kwa jengo la Manzil.

Maafisa hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka kuhusiana na jengo hilo.

TAGGED:
Share This Article