Shule ya sekondari ya wasichana ya St. Georges iliyo kaunti ya Nairobi, imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya mtafaruku kuzuka miongoni mwa wanafunzi.
Kwenye barua iliyoandikwa na usimamizi, wazazi walishauriwa kufika shuleni hapo mapema Ijumaa kuwachukua wanafunzi wao.
Inafahamika kuwa wanafunzi walitishia kuzua vurugu baada ya kutoelewana na walimu ndiposa usimamizi wa shule ukahiari kuwaruhusu kwenda nyumbani.
Kisa hicho ni cha hivi punde huku zaidi ya shue tano zikifungwa na kuwaachilia wanafunzi kwenda nyumbani tangu wiki jana.