Kiungo wa Ghana Enock Morrison wa Gor Mahia alitawazwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Kenya msimu wa mwaka 2025/2026, katika hafla ya kufana iliyoandaliwa Alhamisi usiku katika mkahawa wa Glee.
Morrison aliye na umri wa miaka 26 alikuwa na mchango mkubwa kwa Gor Mahia kutwaa taji la Ligi Kuu msimu uliokamilika maajuzi.
Aidha, Morrison alitawazwa kiungo bora huku akisema tuzo hizo zote zilikuwa kwa heshima ya aliyekuwa mlezi wa klabu ya Gor Hayati Raila Odinga.
Jimmy Owili wa Mara Sugar alitawazwa beki bora, naye Joe Waithera wa Murang’a Seal akatawazwa mfungaji bora wakati Stephen Ochieng wa Shabana akiibuka kipa bora.
Kocha wa Gor Charles Akanor kutoka Ghana, alishinda tuzo ya kocha wa mwaka naye Humprey Aroko wa Kariobangi Sharks akaibuka mchezaji chipukizi bora.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Rais wa FKF Hussein Mohammed na wadau wa ligi kuu pamoja na maafisa kutoka wizara ya michezo.