Ghana na Morocco zatua Marekani tayari kwa Kombe la Dunia

Timu za Taifa za Ghana Na Morocco, zimetua nchini Marekani siku ya Alhamisi wiki moja kabla ya kuanza kwa kipute cha Kombe la Dunia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu za Taifa za Ghana Na Morocco, zimetua nchini Marekani siku ya Alhamisi wiki moja kabla ya kuanza kwa kipute cha Kombe la Dunia.

Morocco,Atlas Lions waliocheza hadi nafasi ya nne mwaka 2022 nchini Qatar,watakita kambi New York New Jersey, ambapo watacheza mechi za kundi C pamoja na Brazil, Scotland na Haiti.

Ghana ambao ni mabingwa wa Afrika mara nne, watakita kambi mjini Boston, ambapo watacheza mechi za kundi L, pamoja na Ureno,Panama na Uingereza.

Fainali za Kombe la Dunia makala ya 23 zitaandaliwa kati ya Juni 11 na Julai 19, katika mataifa ya Marekani, Canada na Mexico.

Share This Article