Timu ya taifa ya Raga ya Kenya kwa wanaume saba upande maarufu kama Shujaa imeanza vibaya katika msururu wa pili wa dunia wa Valladolid, Uhispania, baada ya kupoteza mechi mbili za ufunguzi.
Shujaa inayofunzwa na Kevin Wambua, ilipoteza mchuano wa kwanza wa kundi A mapema Jumamosi alama 10-15, dhidi ya Australia.
Katika mechi ya pili Kenya walinyukwa na Afrika Kusini pointi 14-0, na watarejea uwanjani Jumamosi Adhuhuri dhidi ya Uinereza.
Kinyume na mkondo wa kwana ambapo Shujaa walizoa alama 8 baada ya kumaliza katika nafasi ya 7,matokeo ya mkondo huu yatakuwa duni.
Timu nane bora baada ya mikondo mitatu inayoendelea ya HSBC, zitafuzu kushiriki mashindano ya Dunia msimu ujao.