Ethiopia kuandaa uchaguzi mkuu Juni mosi

Kulingana na tume ya uchaguzi nchini Ethiopia, zaidi ya wapiga kura milioni 50, wamejisajili ikilinganishwa na idadi ya watu ambayo ni milioni 130.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ethiopia itaandaa uchaguzi mkuu Jumatatu ijayo Juni mosi huku Waziri Mkuu Abiy Ahmed,akiwania kuhifadhi kiti chake kwa tiketi ya chama cha Prosperity Party (PP) .

Kampeini zilingia hatua ya lala salama Ijumaa katika mji mkuu wa Addis Ababa,chama tawala cha PP kikifunga barabara kuu ikiwemo eneo la Meskel Square kufanya kampeini za mwisho mwisho.

Kulingana na tume ya uchaguzi nchini Ethiopia, zaidi ya wapiga kura milioni 50, wamejisajili ikilinganishwa na idadi ya watu ambayo ni milioni 130.

Ethiopia inaingia katika uchaguzi huku maeneo mengine yakitarajiwa kukosa kupiga kura kutokana na mizozo kama vile Amhara na Oromia pamoja na mzozo wa eneo la Tigray.

Share This Article