Maafisa wa Shirikisho la Riadha Ulimwenguni wamekuwa nchini tangu mapema juma hili kutathmini ombi la Kenya, kutaka kuandaa mashindano ya Riadha Duniani ya mwaka 2029 au yale ya mwaka 2031.
Ujumbe huo ambao ulikuwa nchini kwa siku tatu ulikutana na uongozi wa chama cha Riadha Kenya ukiongozwa na Rais Jackson Tuwei,wanariadha wastaafu Paul Tergat,Ibrahim Hussein, pamoja na afisa wa kamati kuu ya AK Barnaba Korir.
Kenya inawinda maandalizi ya mashindano ya riadha Duniani baada ya kupoteza maandalizi ya mwaka 2025, kwa mji wa Tokyo nchini Japan.
Maafisa hao kutoka shirikisho la Riadha walitathmini miundombinu kama vile barabara,viwanja na usafiri.
Kenya inawania maandalizi hayo katika uwanja wa Kasarani unaokarabatiwa huku ikishindana na Ethiopia, Uingereza,Italia,Ujerumani,Korea Kusini na India.
Waandalizi wa mashindano ya Dunia ya mwaka 2029 na 2031, atatangazwa Septemba mwaka huu.