Rais William Ruto mapema Ijumaa katika Ikulu ya Nairobi, ametia saini miswada mitatu iliyoidhinishwa na bunge kuwa sheria.
Miswada hiyo ni pamoja na Sheria ya Mwaka 2025 ya Marekebisho ya Uhifadhi na Usimamizi wa Misitu, Sheria ya Kukabiliana Mikasa na ile ya Usawazishaji wa Fedha.
Sheria ya Uhifadhi na Usimamizi wa Misitu inalenga kuhakikisha usimamizi bora wa misitu nchini huku sheria ya mikasa ikitarajiwa kuimarisha kujiandaa kwa Kenya kukabiliana na mikasa punde itokeapo.
Kwa upande wake, Sheria ya Usawazishaji wa Fedha inalenga kuleta usawa wa ugavi wa pesa za umma hususan kwa maeneo yaliyotengwa nchini.