Morara ateuliwa Mkurugenzi Mkuu wa Amnesty International Kenya

Kabla ya uteuzi wake, Morara alifanya kazi kwa zaidi ya miongo mitatu katika uongozi, usimamizi wa mashirika ya umma na uteteaji wa haki za kibinadamu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International Kenya, limemteua George Morara kuwa Mkurugenzi Mkuu wake kuanzia tarehe mbili mwezi ujao.

Morara aliteuliwa kufuatia usaili uliofanywa na atashika hatamu wakati muhimu ambapo shirika hilo linaadhimisha miaka 65 tangu kuasisiwa kwake.

Kabla ya uteuzi wake, Morara alifanya kazi kwa zaidi ya miongo mitatu katika uongozi, usimamizi wa mashirika ya umma na uteteaji wa haki za kibinadamu.

Pia alihudumu katika Tume ya Kitaifa ya kutetea Haki za Binadamu (KNCHR).

Anatwaa uongozi wa Amnesty International Kenya kutoka kwa Irũngũ Houghton, ambaye alijiuzulu baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka minane.

Share This Article