Serikali ya Uganda imetangaza kufunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa kuhofia msambao wa ugonjwa wa Ebola.
DRC imerekodi takriban vifo 220 huku watu wengine zaidi ya 3,000 wakiambukizwa kufikia sasa.
Uganda imechukua tahadhari hiyo baada ya kunakili visa saba vya maambukizi ya Ebola na kifo kimoja jijini Kampala.
Aidha, serikali ya Uganda inaruhusu wageni kutoka DRC kuingia nchini humo kutoa msaada wa dharura kwa waathiriwa.