Odira kushiriki Diamond League kwa mara ya kwanza wikendi hii nchini Morocco

Odira ambaye ni afisa magereza atashiriki mbio za mita 800 kw amara ya pili msimu huu, baada ya kumaliza wa pili katika mashindano ya Kip Keino Classic.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa dunia katika mbio mita 800 Lillian Odira, atashiriki mashindano ya Diamond League kwa mara ya kwanza Mei 31 mjini Rabat Morocco.

Odira ambaye ni afisa magereza atashiriki mbio za mita 800 kw amara ya pili msimu huu, baada ya kumaliza wa pili katika mashindano ya Kip Keino Classic.

,Akioredheshwa wa nne kwenye msimamo wa Dunia,Odira atamenyna na MswiziAudrey Werro ,anayeorodheshwa wa tatu,Addison Wiley wa Marekani ,Prudence Sekgodiso, wa Afrika Kusini na Tsigi Duguma, kutoka Ethiopia.

Mkondo wa Rabat Diamond League, unafuatia mikondo ya shanghai na Xiamen nchini Uchina.

Aidha bingwa wa Dunia na Olimpiki Emmanuel Wanyonyi atatimka mbio za mita 800 mjini Rabat akilenga kuhifadhi taji ya mwaka jana.

Share This Article