Mamelodi Sundowns, almaarufu Masandawana, walijizatiti na kulazimisha sare ya bao moja katika mkumbo wa pili wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumapili usiku mjini Rabat.
Mamelodi walishinda kombe hilo kwa mara ya pili katika historia na la kwanza kwa ushindi wa maboli 2-1, kufuatia sare ya 1-1 jana usiku kuongezea ushindi wa duru ya kwanza.
Masandawana pia ndiyo timu ya kwanza kupokea zawadi ya dola milioni sita za Kimarekani.
Mohamed Hrimat, aliwaweka wenyeji AS FAR uongozini kabla ya Teboho Mokoena kusawazisha kabla ya mapumziko.
Hata hivyo, Hrimat alipoteza penalti ya dakika ya 75 huku Masandawana wakinyakua kombe la pili tangu waliposhinda la kwanza mwaka 2016.