Watu 24 wameripotiwa kufariki katika shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lilitokea katika gari mjini Quetta, nchini Pakistan, siku ya Jumapili.
Watu wengine is 50 walijeruhiwa huku kundi la Balochistan Liberation Army, likikiri kuhusika na shambulizi hilo la Jumapili.
Hali ya hatari imetengazwa katika hospitali za mjini Quetta, wakati madaktari wakiagizwa kuwa katika zamu kushughulikia dharura hiyo.
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif,amelaani shambulizi hilo kupitia ukarasa wake wa X.