Gor Mahia washinda ubingwa wa Ligi Kuu Kenya, baada ya APS kuwafyatua Chui

Ni mara ya kwanza kwa K'ogalo kunyakua ubingwa tangu msimu wa mwaka 2023/2024 kabla ya kupoteza taji msimu uliofuatia kwa Police FC.

Dismas Otuke
1 Min Read

Gor Mahia wametawazwa mabingwa wa Ligi Kuu Kenya kwa mara ya 22 siku ya Jumapili, bila kugusa mpira baada ya wapinzani wa karibu AFC Leopards kushindwa.

Leopards wameikabidhi Gor  kombe baada ya kupoteza mabao 2-1 ugenini Bomet dhidi ya APS.

Gor ambao mchuano wao wa ugenini dhidi ya Mara Sugar katika uwanja wa Raila Odinga kaunti ya Homabay, kusimamishwa na mahakama,wanaongoza jedwali kwa 68, wakisalia ne mechi mbili.

Leopards wanakalia nafasi ya pili kwa alama 64 wakisaza mechi moja.

Ni mara ya kwanza kwa K’ogalo kunyakua ubingwa tangu msimu wa mwaka 2023/2024 kabla ya kupoteza taji msimu uliofuatia kwa Police FC.

Gor Mahia wameshinda ligi miaka ya 1968, 1974, 1976, 1979, 1983, 1984, 1985, 1987, 1990, 1991, 1993, 1995, 2013, 2014, 2015, 2017, 2018, 2018–19, 2019–20, 2022–23, 2023–24 na 2025/2026.

Sirkal sasa watawakilisha Kenya katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Share This Article