Omanyala apiga muda wa kasi sekunde 9.94, Xiamen

Omanyala ameziparakasa mbio hizo kwa sekunde 9.94,akifuatwa na Gift Leotlela wa Afrika Kusini kwa sekunde 10.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Jumuia ya Madola Ferdinand Omanyala, ameendeleza ubora wake msimu huu baada ya kutwaa ushindi wa mita 100 kwa muda bora msimu huu katika mkondo wa Xiamen, Diamond League.

Omanyala ameziparakasa mbio hizo kwa sekunde 9.94,akifuatwa na Gift Leotlela wa Afrika Kusini kwa sekunde 10.

Bingwa wa Dunia na Olimpiki katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji Faith Cherotich, ameambulia nafasi ya tatu kwa dakika 8 sekunde 52.53.

Mbio hizo zimeshindwa naye bingwa wa zamani wa Olimpiki Peruth Jemutai wa Uganda kwa dakika 8 sekunde 51.06,akifuatwa na Winfred Yavi wa Bahrain kwa dakika 8 sekunde 51.54.

Mshindi wa nishani ya fedha ya Dunia Dorcas Ewoi amemaliza wa nne katika mita 1500, zilizoshindwa na Abbey Caldwell wa Australia.

Share This Article