Orlando Pirates ndio mabingwa wa ligi kuu Afrika Kusini

Mara ya mwisho kwa Pirates kunyakua ubingwa wa taji hiyo ilikuwa msimu wa mwaka 2011-2012, wakati huo Benni McCarthy, akiwa mshambulizi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Orlando Pirates ndio mabingwa wa Ligi Kuu Afrika Kusini, kwa mara ya kwanza baada ya subira ya miaka 14.

Pirates wametawazwa mabingwa kufuatia suhindi wa mabao 2-0 dhidi ya Orbit College, katika mchuano wa kufunga msimu siku ya Jumamosi katika uwanja wa Mbombela .

Orbit walihitaji pointi moja pekee ili kujisalimisha lakini kipigo hicho kimewaengua ligini.

Mashabiki wa Pirates wamesherehekea ushindi baada ya kipenga cha mwisho wakitawazwa mabingwa kwa pointi 69,moja zaidi ya watani wao Mamelodi Sundowns waliomaliza wa pili.

Mara ya mwisho kwa Pirates kunyakua ubingwa wa taji hiyo ilikuwa msimu wa mwaka 2011-2012, wakati huo Benni McCarthy, akiwa mshambulizi.

Pirates na Mamelodi wataiwakilisha Afrika Kusini katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao huku Kaizer Chiefs, waliomaliza wa tatu wakishiriki Kombe la Mashirikisho.

Share This Article