Mabanati wa Kenya watoshana nguvu na Waganda

Mechi ya marudio itapigwa jijini Nairobi Mei 30, huku mshindi akifuzu kwa raundi ya tatu .

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 17 iliweka hai matumaini ya kufuzu kwa Kombe la Dunia, kwa mara ya pili baada ya kulazimisha sare ya bao moja dhidi ya wenyeji Uganda katika mkumbo wa kwanza raundi ya pili uliopigwa Ijumaa jijini Kampala.

Mechi ya marudio itapigwa jijini Nairobi Mei 30, huku mshindi akifuzu kwa raundi ya tatu .

Kenya chini ya ukufunzi wa Mildred Cheche inawania kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili baada ya kushiriki fainali hizo mwaka 2024, katika Jamhuri ya Dominica.

Share This Article