Mudavadi: Kenya imejitolea kuwekeza katika Sayansi, Utafiti na Uvumbuzi

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Serikali ya Kenya imeelezea kujitolea kwake kuimarisha uwekezaji katika utafiti, sayansi na uvumbuzi kama hatua ya kusuluhisha changamoto zinazokabili jamii na uchumi.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, amesema serikali inalenga kuongeza ufadhili wa utafiti na uvumbuzi hadi asilimia mbili ya pato jumla la taifa, ili kuimarisha nafasi ya Kenya kama nchi inayoongoza kwa uvumbuzi  barani Afrika.

“Kenya inaendelea kuchukua nafasi yake kuwa miongoni mwa mataifa ya Afrika yanayoongoza katika uvumbuzi,’ alisema Mudavadi.

Kulingana na Mudavadi, Utafiti, Sayansi, Teknolojia na Uvumbuzi, zinasalia nguzo kuu katika kufanikisha mabadiliko ya kiuchumi, ushindani na ukuaji jumuishi wa Kenya.

Aliyasema hayo Ijumaa wakati wa hafla ya kufunga rasmi wiki ya Sayansi, Utafiti, Teknolojia na Uvumbuzi katika Jumba la mikutano ya Kimataifa (KICC).

Wengine waliohudhuria ni pamoja na Makatibu Prof. Shaukat Abdulrazak wa Sayansi, utafiti na Uvumbuzi na Dkt. Beatrice Muganda wa Elimu ya juu.

Share This Article