Zamalek watwaa taji la 15 la Ligi Kuu Misri

Zamalek na Pyramids, watawakilisha Misri katika Ligi ya Mabingwa Afrika, msimu ujao,huku Ahly, na Ceramica, wakicheza mchujo wa kombe la shirikisho.

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Zamalek wamenyakua taji la 15 ya Ligi Kuu nchini Misri baada ya kuwashinda Ceramica Cleopatra bao moja kwa bila katika mchuano wa kufunga msimu Jumatano usiku.

Zamalek waliokuwa wameshindwa kwenye fainali hya Kombe la Shirikisho na USM Alger wiki jana, walihitaji tu sare kwenye pambano hilo ili kuwapokonya taji mabingwa wa mwaka jana Pyramids.

Lilikuwa taji la kwanza kwa Zamalek tangu mwaka 2022, na waliibuka mabingwa kwa kuzoa alama 56,2 zaidi ya Pyramids na tatu juu ya Al Ahly, waliomaliza nafasi ya tatu.

Zamalek na Pyramids watawakilisha Misri katika Ligi ya Mabingwa Afrik msimu ujao huku Ahly na Ceramica wakicheza mchujo wa kombe la shirikisho.

Share This Article