Kenya kumenyana na Guinea,Afrika Kusini na Eritrea kufuzu AFCON

Wenyeji wenza wa AFCON,Uganda wamo kundi H pamoja Botswana,Tunisia na Libya huku Tanzania ikipangwa na Guinea Bissau,Nigeria na Madagascar.

Dismas Otuke
1 Min Read
Harambee Stars yafungana bao 1-1 na Burundi.

Harambee Stars ya Kenya imejumuishwa kundi D, la mechi za kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka ujao.

Kenya itachuana na Afrika Kusini,Guinea na Eritrea, ingawa tayari imefuzu kama waandalizi wenza wa AFCON mwaka 2027.

Wenyeji wenza wa AFCON,Uganda wamo kundi H, pamoja Botswana,Tunisia na Libya, huku Tanzania, ikipangwa na Guinea Bissau,Nigeria na Madagascar.

Timu mbili bora kutoka kila kundi zitafuzu kwa AFCON, ya mwaka ujao huku Tanzania,Kenya na Uganda, wakipata tiketi ya moja kwa moja kama waandalizi.

Share This Article